Na Marco Maduhu
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida mwanamke mmoja aitwaye Elizabeth George mkazi wa Bubale katika wilaya
ya Shinyanga Vijijini amejifungua mtoto wa kike, huku utumbo wake ukiwa nje ya
tumbo.
Mganga mfawidhi wa hospitali
ya mkoa wa shinyanga Dr Fredrick Mlekwa amesema mwanamke huyo amepokelewa
hospitalini hapo majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo, huku akiwa anaumwa
uchungu, ambapo alijifungua mtoto huyo majira ya saa saba usiku.
Akielezea hali hiyo
kitaalam amesema inatokana na kasoro za maumbile au upungufu wa vimelea vya vitamin
kwa mama mzazi wa mtoto huyo na kwamba wanawake wajawazito wanapaswa kuhudhuria
kliniki mapema, ili wataalam waweze kubaini matatizo ya namna hiyo kabla ya
kusababisha madhara zaidi.
Hata hivyo Dr Mlekwa
amesema wamelazimika kumpa rufaa mwanamke huyo ya kwenda katika hospitali ya
rufaa ya Bugando Jijini Mwanza, kutokana na hospitali ya mkoa wa Shinyanga
kutokuwa na wataalamu, ikiwemo vifaa vya kusaidia kumhudumia mtoto huyo.
Social Plugin