Kijana huyo akiwa hoi kwa kipigo baada ya kutupwa porini
Askari polisi wakimsaidia kijana huyo ambae alikuwa hajitambui
WAKATI leo ni
kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
duniani, mkazi mmoja wa ndiuka katika Manispaa ya Iringa ambae jina
lake bado kufahamika amenusurika kifo kwa kupigwa na kundi la
watu wanaojiita kuwa na asila kali wakazi wa Ndiuka akidaiwa ni
kibaka japo habari za nyuma ya pazia zikidai kuwa ni kutokana na wivu
wa kimapenzi
Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ameueleza mtandao huu kuwa
kijana huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mmoja wa
eneo hilo la ndiuka na baada ya kumtosa ndipo mwanamke huyo alipopiga
kelele za mwizi na kupelekea wananchi kumpa kipigo na kumtupa katika
korongo kwenye mlima wa Ipogolo mjini Iringa.
Hata hivyo jitihada za wasamaria wema kuoka maisha yake zilifanyika
kwa kupiga simu polisi na polisi kufika eneo hilo kumuokoa kijana
huyo akiwa hajitambui .
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin