Mwanamme mmoja aitwaye Moshi Andrew (28) mkazi wa kijiji cha Mpera kata ya Isagehe wilayani Kahama mkoani Shinyanga amekutwa akiwa amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kipande cha chandarua.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema mnamo Januari 16 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi walikmkuta mtu huyo akiwa amejinyonga juu ya dari ndani ya nyumba yake kwa kutumia kipande hicho cha chandarua.
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba chanzo cha tukio bado kinachunguzwa na hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Social Plugin