Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi |
MTUHUMIWA wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha
Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari wa FFU
mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)leo ameshindwa kufika
mahakamani katika kesi yake baada ya kudaiwa kuwa ni mgonjwa .
Kesi hiyo ambayo leo ilikuwa ikifikishwa mahakamani hapo kwa ajili
ya kutajwa imeshindikana baada ya mahakama hiyo kuelezwa kuwa
mtuhumiwa huyo ni mgonjwa na imeshindikana kufikishwa mahakamani
hapo.
Mwendesha mashtaka wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza hakimu wa
mahakamani
ya hakimu mkazi wilaya ya Iringa Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa alipaswa
kufikishwa mahakamani hapo leo ila imeshindikana kutoka na taarifa
kuwa ni mgonjwa hivyo kuomba kupangwa tarehe nyingine ya kutajwa
kesi hiyo ambayo bado upelelezi wake kukamilika .
Hata hivyo mahakamani hiyo imeahirisha kesi hiyo hadi Januari 31 itakapotajwa tena .
Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kumuua kwa makusudi kwa bomu aliyekuwa
mwandishi wa habari wa Chanel Tena mkoa wa Iringa marehemu Mwangosi
septemba 2
Septemba mwaka jana katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa
Iringa wakati wa vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Chadema
.kinyume na kifungu cha sheria
namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,
Social Plugin