Mikel Ruffinelli akiwa amekumbatiwa na mumewe |
Kama umesikia wanaume wanaweza kuvunja shingo wakigeuka kumuangalia mwanamke akipita, basi huyu mwanamke atakuwa ameishavunja shingo za wanaume wengi, makalio yake na mahispi yake ya asili yamemfanya awe mwanamke mwenye mahispi makubwa kuliko wanawake wote duniani. |
|
Mwanamama
huyu wa nchini Marekani hajatumia dawa za mchina wala dawa zozote na
ndiye ametambulishwa kuwa ndiye mwanamke mwenye mahipsi makubwa ya asili
kuliko wanawake duniani. Mahispi yake yana mzunguko wa mita 2.44. Mikel Ruffinelli, ambaye ni mama wa watoto wanne akiwa na umri wa miaka 39, mkazi wa Los Angeles amejisifia kuwa maumbile yake yamekuwa yakiwachanganya wanaume wengi. Akiwa na kiuno kidogo kisichoendana na mwili wake cha inchi 40, mahispi yake yana mzunguko mkubwa wa inchi 96. "Nalipenda umbile langu na sina mpango wa kujikondesha kwa diet", alinena Mikel na kuongeza kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake wenye maumbile makubwa sio wale wembamba wembamba. Mikel pamoja na kutamba na maumbile yake hayo ambayo anadai ni urithi toka kwenye familia yake ambapo karibuni ndugu zake wote wa kike nao wana mahispi makubwa. Mikel amelazimika kuishi tofauti ili aweze kuendana na maumbile yake, hawezi kuenea kwenye gari ndogo hivyo gari analoliendesha ni kama lori. Akiwa nyumbani kwake inabidi akae kwenye makochi yaliyotengenezwa kwa chuma badala ya mbao, pia kitanda chake nacho ni futi saba kwa saba. Mume wa Mikel, Reggie Brooks mwenye umri wa miaka 40 ameelezea kupagawishwa na maumbile ya mkewe na ameongeza kuwa kila siku humsifia kwa kumwambia jinsi gani alivyo mrembo. Mikel na mumewe wapo kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa na wamefanikiwa kupata watoto watatu ambapo mtoto wa kwanza wa Mikel alizaliwa katika ndoa yake ya kwanza kabla hajaachika na kuolewa na Reggie. Mikel ameongeza kuwa kwa miaka mitano iliyopita amekuwa akijiingizia kipato chake kwa kupiga picha za mavazi kwaajili ya website ya Big Beautiful Women ambapo katika kila wakati anapoitwa kupigwa picha hulipwa dola 1,000. |
Social Plugin