MKE wa aliyekuwa mcheza filamu mahiri Bongo, marehemu Juma Kilowoko
‘Sajuki’, Wastara Juma amesema kuwa, gari na nyumba vitamuumiza maishani
kwa kuwa ndivyo vitakavyomkumbusha uwepo wa marehemu.
Akizungumza huku akilia kwenye msiba wa mumewe nyumbani kwake, Tabata-Bima, Dar, Wastara alisema yeye na Sajuki waliishi kama mapacha na kila walipokuwa wakitaka kutoka walikuwa pamoja na mara nyingi marehemu ndiye aliyekuwa akipenda kuendesha gari hilo kila walipokuwa wakienda.

“Japokuwa alikuwa akiumwa lakini alipenda aendeshe gari yeye huku akisema mimi nina tatizo la mguu. Mume wangu alinipenda sana jamani, alijitolea kuumia zaidi kwa ajili yangu, nitaliangaliaje hili gari jamani,” alisema Wastara huku akibembelezwa na waombolezaji.
Wastara aliwatoa chozi watu pale aliposema, marehemu alikuwa na kawaida ya kumwambia yeye ni malkia hivyo alitakiwa aendeshwe badala ya kuendesha.
“Sajuki alikuwa akiniambia mimi ni malkia wa nyumba, sitakiwi kuendesha gari, alisema natakiwa kuendeshwa, oooh jamani, nitaishije kwenye hii nyumba mimi,” alisema Wastara huku akizidi kulia.
Sajuki alifariki dunia alfajiri ya Jumatano iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wodi ya Mwaisela kutokana na ugonjwa wa saratani ya ngozi pamoja na uvimbe tumboni.
Alizikwa jana katika Makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.
Social Plugin