Hapa wanafunzi wa IFM wakiandamana kupinga wenzao wawili kuvamiwa na
majambazi halafu wakalawitiwa. Wamekwenda ofisi za makao makuu ya jeshi
la polisi kupeleka malalamiko yao kuwa waliwahi kuripoti kukosa usalama
katika mabweni ao ila jeshi hilo halijachukua hatua zozote.
Wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha IFM wakiwa ofisi za makao
makuu ya jeshi la polisi nchini jijini Dar es salaam leo mchana.
Kiongozi wa wananfuzi iFM akimweleza kamanda wa polisi kanda maalum Dar
es Salaam Suleiman Kova juu ya kadhia iliyowapata wenzao kwa kuvamiwa
na majambazi wakiwa wamelala.
Baada ya kuzungumza nao kamanda Kova aliamua kuandamana nao mpaka zilipo
Hostel na kituo cha polisi walichodai waliripoti matatizo yao lakini
hawakusikilizwa. Kova aliwaahidi watapanda kivuko bila malipo, tatizo
wanafunzi walijaa kuliko uwezo wa kivuko. Hapa akijadiliana na askari
wenzie namna ya kuwapunguza wanafunzi hao....
Wanafunzi hao walivamia makao makuu ya jeshi hilo majira ya saa nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na
jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa
na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya
kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini
suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili
wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi
hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama
mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
Picha zote kwa hisani ya blog ya Said Powa.
Maelezo kidojembe
Social Plugin