Baadhi
ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’,
‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’
na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
PENGINE
haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na
utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika
masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi
wa gazeti hili umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa
mitandao ya kijamii yamechochea ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi
ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya ukahaba vyuoni.
Mitandao
ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna
inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi Jumapili limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi
wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara, kidini,
michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara nyingi huwa wazi
na yeyote anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea ndani.
Mbali
na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi
yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu
mbalimbali nchini.
Uchunguzi
umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia
mitandao wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja
atakayekubaliana na bei waliyoweka.
Baadhi
ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’,
‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’
na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia
katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo
kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia
namba za simu za wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa
utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza
naye kwa kufanya mapatano kabla ya kukubaliana.
Uchunguzi
wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana
kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia
mitandao hiyo.
Baadhi
ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza
kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo
cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Kwa
nyakati tofauti, waandishi wa gazeti hili walitembelea makundi
yanayojinadi kufanya biashara hiyo pamoja na kufanya mawasiliano na
wasichana watatu ambao waliweka picha na namba zao kwenye mtandao.
CHANZO : GAZETI LA MWANANCHI
Social Plugin