Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MJUKUU AUA BIBI YAKE KISHAPU BAADA YA KUKATAA KUFUNDIHWA UCHAWI


Jeshi la polisi mkoani shinyanga linamshikilia kijana mmoja aitwaye Mlaba Hamis (19) kwa tuhuma ya kummua kwa kumpiga nondo kichwani  bibi yake Mindi Doto (70) mkazi wa kijiji na kata ya Ukenyenge tarafa ya Negezi wilayani Kishapu kutokana na kile kinachodaiwa kuwa imani za kishirikina baada ya kijana huyo kukataa kufundishwa uchawi.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SSP Onesmo Lyanga amesema tukio hilo limetokea leo alfajili majira ya kumi na moja ambapo bibi hyo alikutwa chumbani wake akiwa amefariki dunia baada ya kupigwa na mjukuu wake.
Amesema chanzo cha tukio hilo  ni imani za kishirikina baada ya mtuhumiwa kuugua kwa muda mrefu kisha kwenda kwa mganga na kuambiwa kuwa bibi huyo alitaka kumuua kwa kukataa kufundishwa uchawi.
Hata hivyo Kamanda Lyanga amewaasa wananchi kuacha kabisa tabia ya kujihusisha na imani za kishirikina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com