DAWA bandia zinazodaiwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (TB),
zinahofiwa kuingia nchini, ambapo zinadaiwa kutumika kwa kipindi cha
zaidi ya miaka miwili tangu mwaka 2011.
Dawa hizo zinazodaiwa kusambaa katika miji mikubwa
ya Afrika, zinadaiwa kuanza kuleta madhara kwa watumiaji kwani hazina
uwezo wa kuua wadudu wanaosababisha ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wakaguzi
kutoka Marekani,dawa hizo aina ya Rifampicin, Antibiotics simesambaa
katika miji 19 na 7 nchi zilinunua dawa hizo.
Aidha utafiti huo unaonyesha kwamba kumekuwa na
ongezeko kubwa la wagonjwa wa TB ambapo asilimia 6.6 ya Afrika, asilimia
10.1 India na 3.9 asilimia katika Brazil, China, Thailand, Uturuki na
Urusi watu milioni tisa duniani kote huugua TB.
Miji iliyotajwa kununua dawa hizo bandia ni pamoja
na Luanda(Angola),Sao Paulo(Brazil), Beijing(China), Lubumbashi(DRC)na
Cairo(Misri). Miji mingine ni Addis Ababa(Ethiopia), Accra (Ghana), Dar
es Salaam(Tanzania), Delhi na
Kalkata(India),Nairobi(Kenya),Lagos(Nigeria),Moscow(Urusi),Kigali(Rwanda),Bangkok(
Thailand) ,Istanbul(Uturuki),Kampala(Uganda) na Lusaka(Zambia).
Utafiti huo unaeleza pia kwamba,dawa hizo
zinashindwa kufanya kazi kwa asilimia 16.6 asilimia kwa upande wa
Afrika, asilimia 10.1 katika India na 3.9 asilimia katika Brazil, China,
Thailand, Uturuki na Urusi.
Kauli ya TFDA
Akizungumza na gazeti hili ili kuthibitisha
taarifa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Hiit
Sillo alisema kwa sasa hana taarifa yoyote kuhusiana na kuingia kwa dawa
hizo bandia nchini.
Mkurugenzi huyo alilitaka gazeti hili kumtafuta
Ofisa Uhusinao wa TFDA kwa taarifa zaidi,kwani yeye hayupo kazini kwa
kipindi cha wiki moja kwa hiyo asingeweza kutoa ufafanuzi wa suala hilo.
“Siwezi kuzungumza chochote kwani sina taarifa
hizo,ila mnaweza kumtafuta Ofisa Uhusiano kwa majibu zaidi mimi nipo
nyumbani kwa wiki moja sasa naumwa. Pia sina taarifa juu ya suala
hilo,”alisema Sillo.
Gazeti hili lilimtafuta Ofisa Uhusiano wa
TFDA,Gaudensia Simwanza ambapo alisema taarifa hizo hazina ukweli,kwani
kila wakati wanafanya utafiti ili kutambua dawa bandia na hakuna dawa za
kifua kiuu ambazo zimejulikana kama ni bandia kama inavyodaiwa.
Alisema kwa kawaida dawa za kifua kikuu haziuzwi
na badala yake zinatolewa bure sasa kupatikana kwa dawa bandia ni kitu
ambacho hakiwezekani kwani zinatolewa kwa umakini mkubwa.
“Kwanza ni vyema ikafahamika kwamba dawa za kifua kikuu haziuzwi
kwani zinatolewa bure na hazitakiwi kuuzwa, sasa tunashangaa kusikia
dawa hizo zimesambaa nchini kwa kipindi cha miaka mwili,”alisema
Simwanza.
Alisema TFDA ina utaratibu wa kufanya utafiti wa
dawa mbalimbali ikiwa pamoja na dawa za kifua kikuu ambapo kwa kipindi
cha mwaka 2011/12 dawa zote za kifua kikuu zilifanyiwa ukaguzi na hakuna
dawa iliyotambulika kuwa ni bandia.
“Tunautaratibu wa kufanya ukaguzi wa dawa
mbalimbali,ambapo mwaka jana na mwaka juzi tulifanya ukaguzi wa dawa
zote za kifua kikuu na hakuna dawa ambazo zilikutwa ni bandia kama
inavyodaiwa. Sasa taarifa kama hizo sio za kweli na Watanzania wasiwe na
wasiwasi,”alisema.
CHANZO: MWANANCHI