Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MGEJA AMLIPUA MBOWE

Jeshi la polisi nchini limeshauriwa kuchukua hatua za kumfikisha
mahakamani  mara moja mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ili akathibitishe ushahidi alionao kuhusu tuhuma alizoibua dhidi ya Jeshi hilo kwamba linahusika katika tukio la kuripua bomu hivi karibuni mkoani Arusha.

 
Ushauri huo umetolewa Juzi na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani
Shinyanga Khamis Mgeja alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ufala kata ya Kilago wilayani Kahama mkoani shinyanga, uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata hiyo wakiwemowanachama wa CCM,Katibu mwenezi wa CCM mkoa , wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Kahama na watendaji wa kata za Kilago la Iyenze.

Mgeja alisema kitendo cha Mbowe kukataa kukabidhi ushahidi anaodai kuwanao ukimuonesha mtuhumiwa wa tukio la ulipuaji bomu katika viwanja vya Soweto mkoani Arusha uliosababisha vifo vya watu watatu akishinikiza kuutoa mpaka pale Rais Jakaya Kikwete atakapokuwa ameunda tume huru hakiashiri kuwepo kwa amani nchini.


Alisema Mbowe anapaswa kufikishwa mahakamani mara moja ili ukweli upatikane na kwani yeye ndiyo anawajua wahusika huku pia akilishauri jeshi hilo la polisi kutengua kusudio lake la kutoa zawadi ya shilingi milioni 100 kwa mtu atakayemtaja mtuhumiwa wa tukio hilo la Arusha kwa vile tayari kuna mtanzania aliyetangaza kuwa anao ushahidi
wote.
 
Mgeja alisema fedha iliyoahidiwa na Paul Chagonja ni vizuri sasa kama haina kazi nyingine ielekezwe kwenye huduma zakijamii kama vile kununua dawa za hospitali au zikatengeneze madawati ya watoto katika shule za msingi na zile za sekondari.
 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com