Mwili wa mtoto aliyebakwa na kuuawa kisha kuwekwa kwenye boksi |
Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka
kati ya kumi na mbili hadi kumi na tatu,mwenye jinsia ya kike,asiyefahamika
jina wala makazi yake amekutwa akiwa ameuawa katika eneo Ngokolo mitumbani
karibu na jalala la takataka mjini shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga ACP Evarist
Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana maiira ya saa tano
asubuhi na kuongeza kuwa mtoto huyo mwenye jinsia ya kike alikutwa akiwa ameuawa
kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kisogoni kisha mwili wake kuwekwa kwenye
boksi na kufungwa kwa kamba za katani.
Kamanda MangallA amesema uchunguzi wa
daktari unaonesha kuwa mtoto huyo alibakwa kabla ya kuuawa na kuongeza kuwa
jeshi la polisi bado linaendelea kufanya uchunguzi ili kuwabaini na kuwakamata
watu waliohusika katika mauaji hayo kwani mpaka
sasa chanzo cha mauaji hakijulikani.
Kamanda wa polisi mkoani hapa anatoa wito
kwa wananchi kutoa taarifa za siri kwa jeshi hilo ili kuweza kuwabaini na
kuwakamata watuhumiwa wa tukio hilo.
Social Plugin