Awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya umeme nuru kwa washiriki,huyu ni Wakala wa Nishati Vijijini (REA)mtaalam Mshauri Mzumbe Musa akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi hapo juzi
Mkuu wa wilaya akizindua mafunzo kwa waendelezaji wa nishati vijijini ambapo alisema uzoefu
unaonesha kuwa waendelezaji wa nishati vijijini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
nyingi kama vile ukosefu wa mitaji,utaalamu mdogo wa kiufundi na ugumu wa
kupata mikopo kwenye benki za kibiashara na riba kubwa zinazoambata na mikopo
hiyo
Kushoto ni Wakala wa Nishati Vijijini ,ambaye ni mkufunzi katika mafuzo hayo akifuatilia hotuba ya ufunguzi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya
Hotuba inaendelea katika ukumbi wa Nedman Hotel mjini Shinyanga
Kulia ni Bwana Monga Paschal Edward ,akiwa na washiriki wengine akifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya
Picha ya pamoja ya washiriki na mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Pamoja na kuwepo kwa sera ya taifa ya nishati inayolenga
katika upatikanaji wa nishati bora kwa lengo la kukuza uzalishaji mali na
kuendeleza huduma za jamii,uzoefu umeonesha kuwa waendelezaji wa nishati
vijijini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa
mitaji,utaalamu mdogo wa kiufundi na ugumu wa kupata mikopo kwenye benki za
kibiashara na riba kubwa zinazoambata na mikopo hiyo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose
Nyamubi wakati akifungua mafunzo ya umeme nuru katika ukumbi wa Nedman Hotel
mjini Shinyanga yaliyoandaliwa na wakala
wa nishati vijijini ambapo washiriki wapatao 16 kutoka maeneo mbali mbali
nchini,wanashiriki mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda siku 9 kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa kufunga umeme na mitambo katika maeneo ya vijijjini.
Alizitaja changamoto zingine kuwa ni uharibifu wa mazingira
pamoja na waendelezaji hao wa nishati vijijini kutojua au kutokuwa na uhakika
wa fursa mbalimbali zilizopo katika uwezeshaji wa kuanzisha na kusimamia miradi
ya nishati vijijini.
Hata hivyo bi Nyamubi
alisema wadau wa nishati vijijini
wanaweza kukabiliana na changamoto hizo kwa kushirikiana na wakala wa nishati
vijijini na taasisi zingine za mambo ya nishati na mazingira zilizopo ndani na
nje ya nchi huku akiongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia katika kutoa mwanga
zaidi juu y fursa zilizopo katika kupata ruzuku na mikopo yenye riba na
masharti nafuu itakayowezesha kuwekeza katika sekta ya nishati na taarifa juu
ya taasisi wanazoweza kuashirikiana nazo ili kuondoa changamoto hizo
Kwa upande wake wakala wa nishati vijijini,ambaye ni
mtaalamu mshauri bwana Mzumbe Musa alisema kuwa mafunzo hayo yatakayodumu kwa
muda wa siku 9 yanalenga kuendeleza miradi ya umeme nuru vijijini ambapo
washiriki watajifunza kwa vitendo na nadharia namna ya kufunga umeme na
mitambo.
“Tayari tumewajengea uwezo katika maeneo mbalimbali nchini
mfano huko Iramba na Mkuranga lakini hapa Shinyanga pamoja na mambo mengine
washiriki wa mafunzo haya watashiriki katika zoezi la kufunga umeme katika
shule ya sekondari Mwamalili iliyopo ndani ya manispaa ya Shinyanga”,alisema
Musa.
Bwana Musa aliongeza kuwa wakala wa nishati
vijijini wameandaa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo washiriki hao ambao
wamepatikana kwa njia ya matangazo kwenye vyombo vya habari kisha kutuma maombi
ya kupatiwa mafunzo hayo wakiwa kama sehemu ya wadau muhimu sambamba na
kuhamasisha matumizi ya nishati bora hasa katika maeneo ya vijijini lakini pia
kama njia ya kupata ajira.
Social Plugin