viongozi wa chadema wakiingia katika viwanja vya mahakama ya mwanzo eneo la Nguzo nane tayari kwa mkutano hapo juzi
Mkutano umeshaanza waliovaa nguo nyekundu ni redbrigades kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama kwa viongozi wao na wananchi katika mkutano huo
mkutano unaendelea
hali ndivyo ilivyokuwa
Mwenyekiti wa chadema taifa mheshimiwa Freeman Mbowe akihutubia wananchi wa mkoa wa shinyanga ambapo aliwaomba kuwa makini na mambo matano wakati mchakato wa kupata katiba ukiendelea ,mambo hayo ni maadili kwa viongozi,suala la serikali tatu,haki za binadamu,mabaraza ya katiba na tunu za taifa kama vile uwazi na ukweli katika mikataba ili kuwabaini wanaoiibia nchi
wananchi wakiwa wamenyosha mikono baada ya kuambiwa na mwenyekiti wa chadema kama wanaunga mkono kwamba chama chake kiendelee kutoa mafunzo kwa vijana wa redbrigades au la! kwa ajili ya usalama wa viongozi wao na wananchi kwa ujumla lakini pia kama wanaunga mkono suala la serikali tatu kuingizwa kwenye katiba
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin