KATIBU MKUU TUGHE TAIFA ALLY KIWENGE AFANYA ZIARA YA GHAFLA SHINYANGA
Friday, July 12, 2013
Katibu mkuu wa TUGHE taifa amefanya ziara ya siku mbili mkoani shinyanga na kuzungumza wa watumishi wa umma katika ukumbi wa NSSF uliopo mjini shinyanga kisha kuelekea katika hospitali ya mkoa huo na kuzungumza na madaktari ,manesi na wauguzi wa hospitali hiyo hapo jana leo yupo mkoani Simiyu akiendelea na ziara yake
Katibu mkuu wa wanachama wa Chama Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya Tanzania
(TUGHE)Ally Kiwenge akiwa mkoani Shinyanga,wakati wa ziara ya siku mbili ,akifuatilia kwa umakini na kuhuzunishwa na kero zinazowakabili wafanyakazi ikiwemo kucheleweshewa mishahara na kukatwa makatao bila ridhaa yao ,alipofanya kikao na wanachama hao
katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga.
Ally
Kiwenge akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka aliwataka waajiri baada ya kupokea malalamiko mengi dhidi yao ,kujichunguza na kuacha mara moja tabia ya
kuwalazimisha wafanyakazi kufanya wanavyotaka wao kinyume cha sheria na maadili
ya kazi huku pia akikemea tabia ya baadhi ya waajiri kuficha posho za
wafanyakazi wao.
·Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga Dk Fredrick
Mlekwa akifuatilia hotuba ya katibu mkuu TUGHE taifa hapo jana ambapo alisema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa na hospitali hiyo kama vile
kupungua kwa idadi ya vifo kwa wagonjwa wanaolazwa,kupngua kwa vifo vya akina
mama na watoto na kupungua kwa malalamiko ya wananchi,alizitaja pia
changamoto zinazoikabili hospitali hiyo kuwa ni pamoja na uhaba wa
watumishi,ukosefu wa nyumba za watumishi ,upungufu wa dawa na ukosefu wa gari
la kusafirishia watumishi
·
Viongozi TUGHE mkoa wa Shinyanga
Kiwanga akizungumza na watumishi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga
Watumishi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga wakimsikliza katibu wao hospitalini hapo ambapo walieleza kukerwa na hali ya kucheleweshewa mishahara:PICHA ZOTE NA KADAMA MALUNDE
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin