Baadhi ya wanaume katika jamii wanakabiliwa
na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia kutokana na uoga,aibu na hofu ya kuonekana
wanyonge kama jamii itafahamu changamoto hiyo
katika familia yake, ikwemo kuachika bila sababu za msingi na kunyimwa tendo la
ndoa na wake zao.
Afisa Ustawi wa
Jamii mkoa wa Shinyanga,bwana Songelaeli Daniel ameiambia blog hii kuwa sio wanawake pekee
wanaonyanyasika kijinsia, bali pia kuna baadhi ya wanaumme ambao wamekuwa
wakinyanyasika kutokana na uoga na aibu ya kuonekana hawafai katika jamii hivyo
hulazimika kukaa kimya.
Alisema hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wanawake mkoani humo
kuhusu mambo ya kijinsia tofauti na siku za nyuma,ambapo sasa wanawake wanafika
kwa wingi katika ofisi hizo kueleza shida zao,
,lakini wanaumme ni mara chache
sana wakati wapo baadhi yao wanaachika bila sababu za msingi na wengine kunyimwa unyumba.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Haki za Wanaume
Tanzania(TAMRA),bwana Anthony Sollo amesema wanaume wananyanyasika kijinsia
kutokana na imani iliyojengeka katika jamii kuwa mwanamme ndio kichwa cha
familia hivyo kuongea mbele ya jamii kuwa wananyanyaswa hufikiri kuwa ni kitendo cha ajabu na kwamba wataonekana wako chini ya wanawake
kitendo ambacho huona kama wataonekana wanyonge na kuchekwa na jamii
inayowazunguka.
Amesema wanaume wanatakiwa sasa kukitumia chama cha wanaume Tanzania kuhakikisha kuwa wanapata haki zao za
msingi ikiwemo kusikilizwa katika vyombo mbalimbali vya maamuzi kama vile mahakama,jeshi la polisi na mabaraza mbalimbali
yanayohusika na usuluhishi wa mambo ya ndoa.
Social Plugin