BI Martha Kapuya (104) mkazi wa kijiji cha Uzogore Bujiga Enzi za uhai wake baada ya kuanza kulelewa na Askofu MWOMBEKI akiwa ni miongoni mwa vikongwe 108 anaowalea katika manispaa ya Shinyanga waliojitenga na jamii kwa hofu ya kuuawa kutokana na imani za kishirikina
Mwili wa marehemu Martha Kapuya aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 104 ukiwa kwenye jeneza kabla ya mazishi hapo jana nyumbani kwake katika kijiji cha Uzogore Bujiga ndani ya manispaa ya shinyanga
Watu wenye mapenzi mema waliohudhuria mazishi ya bi Martha aliyekuwa akilelewa na Askofu Mwombeki wa Kanisa la Emmanuel,ambapo kabla ya hapo alikuwa anaishi mjini shinyanga kwa kuombaomba na alikimbia makazi yake kwa hofu ya kuuawa kutokana na imani za kishirikina kwani alikuwa na macho mekundu.
Askofu Mwombeki akiongoza ibada ya mazishi katika kijiji cha Uzogore Bujiga ambapo aliiomba jamii kuwajali wazee ili waweze kuishi maisha marefu kama ilivyokuwa kwa bibi Martha ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 104 kutokana na umri wake kuwa mkubwa lakini kabla ya hapo alikuwa ametengwa na jamii lakini askofu huyo akachuchua jukumu la kumlea akiwa ni miongoni mwa vikongwe 108 anaowalea katika manispaa ya shinyanga.
Social Plugin