Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MHITIMU WA UDOM ALIYEFARIKI GHAFLA


Marehemu Zuhura Mashaka(23) aliyehitimu  shahada ya elimu ya miamba madini UDOM, Juni 28 mwaka huu na kufariki dunia Julai 14 mwaka huu, enzi za uhai wake



umati wa watu katika eneo la makaburi ya familia wakisubiri kumzika mpendwa wao katikati ni Padre Emmanuel Makolo wa Parokia ya Busanda aliyeongoza ibada ya mzishi nyumbani kwa marehemu..




Kushoto ni Richard Kabega akiwa na Said Nassoro wahitimu wa mwaka 2005 katika shule ya sekondari Kituli wakiwa eneo la msiba.

Baba wa marehemu Mzee Mashaka akiwa na mke wake wakiweka shada la maua katika nyumba ya marehemu




Walimu wa shule ya msingi Kituli wakiweka shada la maua



Walimu wa shule ya sekondari Kituli baada ya kuweka shada la maua.


Kushoto ni mheshimiwa Azza Hilal mbunge wa viti maalum jimbo la solwa akizungumza mara baada ya mazishi ambapo alisema Zuhura alikuwa kijana mwenye uwezo mkubwa darasani ambapo takwimu zinaonesha kuwa ndio msichana wa kwanza kupata daraja la kwanza katika shule ya sekondari kituli tangu ianzishwe mwaka 1997,na kuongeza kuwa kifo chake ni pigo kubwa sio tu kwa familia bali taifa kwa ujumla.
Zuhura kazaliwa 1990 akasoma kituli shule ya msingi,baadaye,kituli sekondari ,akaenda nganza sekondari,akafundisha St Hellen DSM, baadae UDOM,

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com