MBUNGE AZZA HILAL AONGOZA MAMIA YA WATU MAZISHI YA MHITIMU WA UDOM ZUHURA MASHAKA
Wednesday, July 17, 2013
Marehemu zuhura mashaka mhitimu wa UDOM enzi za uhai wake
Padre Emmanuel Makolo wa Parokia ya Busanda
akiongoza ibada ya mzishi nyumbani kwao na marehemu
-Kushoto ni Richard Kabega akiwa na Said Nassoro wahitimu wa
mwaka 2005 katika shule ya sekondari Kituli wakiwa eneo la msiba.
Baba wa marehemu Mzee Mashaka akiwa na mke wake
wakiweka shada la maua
katika nyumba ya marehemu
Walimu wa shule ya msingi Kituli wakiweka shada
la maua
Walimu wa shule ya sekondari Kituli baada ya
kuweka shada la maua
Wanafunzi waliosoma na marehemu katika shule ya
sekondari kituli baada ya kuweka shada la maua
mheshimiwa Azza Hilal mbunge wa viti maalum jimbo la solwa
akizungumza mara baada ya mazishi ambapo alisema Zuhura alikuwa kijana mwenye
uwezo mkubwa darasani ambapo takwimu zinaonesha kuwa ndio msichana wa kwanza
kupata daraja la kwanza katika shule ya sekondari kituli tangu ianzishwe mwaka
1997,na kuongeza kuwa kifo chake ni pigo kubwa sio tu kwa familia bali taifa
kwa ujumla
Zuhura Mashaka alizaliwa katika kijiji cha Kituli wilaya ya
shinyanga mwaka 1990 akasoma katika
shule ya Msingi na shule ya sekondari Kituli zilizopo katika kijiji hicho,
mnamo mwaka 2008 hadi 2010 akajiunga na
shule ya sekondari Nganza iliyopo mkoani
Mwanza kwa masomo ya kidato cha tano na sita,na baadae kujiunga na Chuo kikuu cha Dodoma na kuhitimu
Juni 28 mwaka huu akiwa na shahada ya
elimu ya miamba madini(Geology).
Baada ya kumaliza masomo yake alikwenda nyumbani kwao Kituli Julai 5 mwaka
huu,na mnamo Julai 13 alisafiri kwenda mkoani Geita kutafuta kazi katika mgodi
wa madini wa Geita(GGM) na kufikia nyumbani kwa kaka yake anayeishi mkoani
humo.
Akiwa kwa kaka yake siku iliyofuata tarehe 14 Julai ghafla
alianguka na kuanza kutoa mapovu mdomoni kisha kukimbizwa hospitali ambapo muda
mchache tu akaaga dunia.
.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin