NB..SIYO PICHA YA MTOTOALIYEUAWA |
Ni Siku chache tu baada ya mtoto kubakwa ,kuuawa kisha mwili
wake kuwekwa kwenye boksi na kutupwa karibu na dampo la taka eneo la Ngokolo
Mitumbani katika manispaa ya shinyanga,.
mtoto Jamila Ramadhani mwenye umri wa miaka minne ameuawa
kikatili kwa kupigwa na fimbo na kipande cha bomba la maji cha plastiki kichwani na mama wa kambo aitwaye Moshi Kasema mwenye
umri wa miaka 35 aliyekuwa anaishi naye katika eneo la Mshikamano katika
manispaa ya shinyanga kisha kukimbia kusikojulikana.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga kamishina
msaidizi wa polisi Evarist Mangalla tukio hilo limetokea jana
majira ya saa kumi na mbili na
dakika 37 na kuataja chanzo cha tukio
hilo kuwa ni mtoto Jamila Ramadhani kujisaidia bila kujisafisha
Social Plugin