Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA KIJIJI AMNYONGA HAWARA YAKE




Nyamizi Elias Salamba (28) mkazi wa Kijiji cha Ilomelo kata ya Ulowa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kunyongwa shingo na mwanamme mwanamme anayedaiwa kuwa ni mwenyekiti wa kijiji cha Kasela wilaya ya Nzega mkoani Tabora kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamme mwingine.

Tukio hilo limetokea juzi katika kijiji cha Ilomelo wilayani Kahama majira ya saa nne usiku ambapo mwanamke huyo alinyongwa shingo na hawara yake aliyejulikana kwa jina la Kashindye Abeid Sheni  mwenye miaka 45 ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Kasela kilichopo mkoani Tabora.
Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga linamshikilia mtuhumiwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com