Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NKULILA AULAMBA TENA UNAIBU MEYA MANISPAA YA SHINYANGA WAKATI WA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA MANISPAA HIYO

Baraza la madiwani wa manispaa ya shimyanga likiendelea jana katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa shinyanga

Diwani wa viti maalum Shella Mshandete akisisitiza suala la ujenzi wa vyoo katika shule za manispaa kupewa kipaumbele zaidi

Aliyesimama ni Kaimu mkurugenzi mamlaka ya maji safi na maji taka katika manispaa ya shinyanga -SHUWASA ,Injinia Silvester Kihole akizungumzia suala la malipo ya ya shilingi elfu mbili kwa wateja wao kila mwezi ambapo alisema pesa hiyo sio gharama halisi bali ni sehemu tu ya mchango wa wananchi ili huduma iendelee kutolewa.Aliyekaa ni afisa uhusiano SHUWASA bi Nsianeli Gelard wakati baraza la madiwani likendelea

Kulia aliyesimama ni mkuu wa wilaya ya shinyanga Bi Anna rose Nyamubi akizungumzia suala la malipo ya shilingi elfu mbili za wateja wa SHUWASA ambapo alisema  suala hilo lifanyiwe utafiti na kama itabainika kuwa hiyo pesa ni kubwa basi iondolewe kuepuka kuwaumiza wananchi

Kushoto ni Mstahiki meya manispaa ya shinyanga Gulam Hafidh Abubakar Mukadam akiwashukuru madiwani wa manispaa kwa ushirikiano wao tangu aondoke kwa muda mrefu kwenda kutibiwa India kwa maradhi yaliyokuwa yanamsumbua na kusema kwamba sasa anaendelea vizuri

Mstahiki meya akimtangaza ndugu David Mathew Nkulila ambaye ni diwani kata ya Ndembezi kupitia CCM kuwa mshindi katika uchaguzi wa kiti cha Naibu meya baada ya kupata kura 14 dhidi ya mpinzani wake Nyangaki Shilungushela,ambaye ni diwani wa kata ya Kambarage kupitia CHADEMA aliyepata kura 8.


wa tatu kutoka kushoto ni ndugu Nkulila akirudi kwenye kiti chake huku akifurahia ushindi

Kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya shinyanga Festo Kang'ombe akimpa mkono naibu meya mshindi
Naibu meya Nkulila akitoa shukurani baada ya ushindi na kurejea kwa mara nyingine ya pili katika nafasi hiyo ambapo aliwaasa madiwani  kuweka pembeni itikadi za kichama pembeni na kufanya kazi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com