AIBU TUPU!!! SHULE YA BUGOYI IKO MJINI SHINYANGA VYOO VIBOVU,WANAFUNZI WANAKAA CHINI



NJE YA CHOO CHA WANAFUNZI-Mapema jana Kamati ya shule ikiangalia eneo la nje ya choo cha wanafunzi ambapo wanafunzi wanalazimika kujisaidia kwa kuogopa kutumbukia chooni kwani vyoo hivyo vina nyufa kubwa. Kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Bugoyi B ya mjini Shinyanga

Rweshabura Anord,aliyeshika kiuno ni afisa mtendaji wa kata ya Ndembezi iliko shule hiyo James Dogani.Hapo jana wakati wa kikao cha kamati ya shule,hapa wanajionea halisi ya mazingira ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo




Huu ni ukuta wa choo cha wanafunzi
katika shule ya msingi Bugoyi B iliyopo katika manispaa ya Shinyanga

Nyufa za hatari hapo sakafuni
 choo cha walimu


Hapa kamati inajadili namna ya kuondoa matatizo yaliyopo shuleni hapo ambapo waliomba taasisi na mashirika mbalimbali kuweka nguvu zao kwenye shule hiyo

 KUMBE HATA  MAWE YAPO!- darasa linaendelea


Darasa linaendelea wanafunzi wako chini katika moja ya madarasa ambako kamera ya mwandishi ilinasa kilichokuwa kinaendelea

 mwalimu yuko kazini
shule hiyo ilijengwa mwaka 2004 ikiwa namba ya usajili P/S 039 mbali na kukabiliwa na tatizo la uhaba na ubovu wa vyoo
ina wanafunzi 865 wanatumia matundu 7 ya choo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post