MWANAMME ASIYEFAHAMIKA AKUTWA AMEKUFA NDANI YA DIMBWI KARIBU NA BWAWA LA NING'WA
Tuesday, August 13, 2013
NB: SIYO DIMBWI ALIKOKUTWA MAREHEMU
Mwanamme ambaye hajafahamika jina kabila wala makazi yake mwenye umri 35-45 amekutwa amefariki na mwili wake ukiwa ndani ya dimbwi la maji lililopo karibu na bwawa la maji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Evarist Mangalla,tukio hilo limetokea jana majira ya kumi jioni katika eneo karibu na bwawa la Ning'wa lililopo katika kijiji na kata ya Chibe,tarafa ya Old Shinyanga ndani ya Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda Mangalla amesema chanzo cha tukio bado hakijafahamika.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin