ASASI YA YHDA YA SHINYANGA YAENDESHA MJADALA WA RASIMU YA KATIBA MPYA TINDE -SHINYANGA
Tuesday, August 27, 2013
Mwanasheria wa wilaya ya
Shinyanga Saleh Hassan akitoa mwongozo kwa wakazi wa Kijiji cha Tinde katika
kata ya Tinde mapema jana katika Ukumbi wa TRC uliopo eneo hilo karibu na shule
ya msingi Tinde ambapo alisema mjadala utalenga zaidi aina ya muungano ambao
wananchi wanautaka,ambapo mjadala utadumu kwa muda wa siku tatu yaani Agust 26
hadi 28 mwaka huu.
Wakazi wa Tinde waliojitokeza katika
mjadala wa rasimu ya katika mpya ambapo pamoja na mambo mengine walipendekeza katiba itaje wazi kuwa ndoa za jinsia moja ni marufuku
Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake
kuhusu aina ya muungano inayotakiwa ambapo alipendekeza kuwepo serikali tatu
kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu ya katiba mpya 2013.
Mratibu wa asasi ya kiraia
Youth
Health and Development Association YHDA,bwana Rigobert Rweyombiza aliwataka washiriki katika baraza hilo
kutoingiza itikadi za kisiasa au dini kwani katiba itakayopatikana ni kwa
maslahi ya watanzania wote.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin