Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DIWANI AJICHOMA MKUKI ,ASEMA POSHO YAKE ITUMIKE KUNUSURU WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BUGOYI B YA MJINI SHINYNGA WALIOKO HATARINI KUTUMBUKIA CHOONI


Afisa elimu ufundi wa manispaa ya Shinyanga Mhela Mohammed akizungumza JANA JIONI katika kikao hicho ambapo alisema kinachotakiwa ni ujenzi wa vyoo vipya badala ya kukarabati vyoo ili kunusuru maisha ya wanafunzi ambapo wako hatarini kutumbukia kwenye vyoo hivyo lakini pia aliwaomba wazazi kuchangia maendeleo ya shule ikwemo kununua madawati na kuwapatia huduma ya uji wanafunzi

Mmoja wa wazazi wa watoto wa shule ya msingi Bugoyi  B John Shashu akichangia mawazo katika kikao cha wazazi ambapo yeye alisema atatoa mabati mawili kuchangia ujenzi wa choo shuleni hapo ambayo vina nyufa na mipasuko mikubwa.
Katikati ni Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila kupitia CCM,ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga akisistiza jambo wakati wa kikao cha wazazi  ambapo alisema Posho ya diwani ni shilingi laki mbili na nusu kwa mwezi,hivyo alijitoa mhanga na kusema kuwa atajinyima kwa miezi miwili ili hiyo laki 5,achangie ujenzi wa vyoo vya watoto wao,na kuwaomba wazazi kumuunga mkono,huku akiongeza kuwa ifike mahali wazazi wawahurumie watoto na kutambua  kuwa haki ya watoto iko mikononi mwa wazazi
Baadhi ya wazazi waliohudhudhuria kikao hicho ambapo
 pamoja na wazazi kufanya harambee kuchangia ujenzi wa choo,pia walikubaliana kila mzazi kuchangia shilingi elfu 20 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo,kutengeneza madawati 150,na huduma ya uji kwa wanafunzi.

KIKAO HICHO CHA WAZAZI KIMEFANYIKA SIKU CHACHE TU BAADA YA MTANDAO HUU WA MALUNDE1.BLOGSPOT.COM KURIPOTI KUHUSU HATARI YA WANAFUNZI WANAOSOMA KATIKA SHULE HIYO KUTUMBUKIA KATIKA VYOO AMBAVYO KUTA ZAKE ZIMEPASUKA NA SAKAFUNI KUNA NYUFA ZA HATARI HUKU WANAFUNZI WAKILAZIMIKA KUKAA CHINI WAKATI WA MASOMO KUTOKANA NA UPUNGUFU WA MADAWATI JAPO SHULE HIYO IKO MJINI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com