Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya |
Mkazi wa kitongoji cha Mwankumbo kijiji cha Zobogo kata ya Itwangi
tarafa ya Itwangi wilaya ya Shinyanga Shija
Mfuko Jondo(57) amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba ya katani juu ya mti
wa mwembe katika shamba la mapera katika eneo la Nhumbili lililopo kata ya
Tinde wilaya ya shinyanga
Mtoto wa marehemu aitwaye Shija Mathias ameiambia malunde1.blogspot.com
kuwa baba yake alikuwa amefanyiwa oparesheni ya tumbo mwezi Juni mwaka huu,na
tayari alikuwa akifanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuimarisha afya yake ila
siku hiyo aliaaga asubuhi kuwa anakwenda kufanya mazoezi na hakurudi.
Alisema walimkuta mzee huyo amejinyonga
kwenye shamba la mapera hapo juzi jioni
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya
Kihenya amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo chake bado
hakijafahamika ingawa marehemu alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.
Social Plugin