Makaburi ya waislam
ya Nguzo Nane mjini shinyanga,japokuwa yamezungushiwa ukuta lakini katika baadhi ya maeneo
hakujazibwa na kusababisha baadhi ya watu wanaoishi kando kando ya eneo hilo kutupa uchafu katika makaburi
hayo ambapo ni wakati mzuri sasa kuachana na tabia hiyo kama walivyoeleza viongozi wa dini ya kiislam waliofika hapo jana wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kushughulikia makaburi hayo
Wa pili kutoka
kushoto ni mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiwasili katika eneo
la makaburi ya Nguzo nane mjini shinyanga hapo jana,tayari kwa uzinduzi wa
mfuko wa kushughilikia makaburi hayo.Mkuu huyo wa mkoa alisema mfuko huo
utasaidia sana kwani watu wasio na uwezo watazikwa bure huku wengine
wakichangia kiasi flani.Mbali na hayo alipompongeza mbunge wa kishapu kwa
kushiriki katika shughuli za kijamii kwani huo ndio upendo wa dhati kwa
wananchi na jamii kwa ujumla.
Sheikh Nassoro Said
Elmaamry kutoka Jumuiya ya East Qaama Tanzania akitoa neno wakati wa uzinduzi
wa mfuko wa kushughulikia shughuli za makaburi ya Waislam ya Nguzo nane,ikiwa
ni jitihada za mbunge wa jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mheshimiwa Suleiman
Nchambi kwa kushirikiana na viongozi wengine akiwemo sheikh mkuu wa mkoa wa
shinyanga.Sheikh Nassoro alionesha kufurahia
kitendo cha mbunge huyo kushiriki kwa moyo mmoja katika shughuli za
kijamii
Mbunge wa kishapu
suleiman Nchambi akisoma taarifa kuhusu jengo maalum kwa ajili ya kushughulikia
miili ya marehemu ambapo alisema katika eneo hilo taarifa mbalimbali za watu
waliozikwa pale zitakuwepo,taarifa za misiba na mazishi zitapitia pale na
usimamizi wa makaburi hayo lakini pia akieelezea kuhusu mfuko wa kushughulikia
makaburi ya Nguzo nane ambapo alisema jamii inapaswa kujenga tabia ya
kutembelea makaburi na kuyathamini
Sheikh mkuu wa mkoa
akizungumzia kuhusu kifo kwamba kila mwanadamu lazima atapitia makaburini ikiwa
ni njia ya kuelekea ahera yaani kwa mungu aliyetuumba hiyo tukiwa hai yatupasa
kujiandaa kwa kutenda mema hapa duniani
Hapa anawaeleza waumini wa dini ya kiislam umuhimu wa kutembelea makaburi kwamba mtu akitembelea makaburi anakuwa anakumbuka ahera
Aliyevaa nguo nyeusi
ni Mbunge wa Kishapu alifuatilia maneno kutoka kwa sheikh mkuu wa mkoa
Sheikh mkuu wa mkoa
akihamasisha watu waliofika eneo hilo kuchangia mfuko uliozinduliwa ambapo
zaidi sh milion 9 zilipatikana baada ya kufanyika kwa harambee hiyo,ambapo
viongozi akiwemo mkuu wa mkoa wa shinyanga walichangia mfuko huo
waumini wa dini ya
kiislam wakifuatilia kilichokuwa kinaendela katika eneo hilo la makaburi
Waumini wa dini ya kiislam wanafuatilia kinachoendelea
Sheikh mkuu wa mkoa wa shinyanga Ismail
Makusanya akionesha sanda ilifungwa tayari kutumika ambayo ni moja ya vitu
vitakavyokuwa vinapatikana katika jengo maalum kwa ajili ya kuhifadhia na
kuandaa maiti lililopo katika eneo la makaburi ya waislam ya Nguzo nane mjini
Shinyanga,ambalo lilikuwa linatumika tangu mwanzo lakini kwa sasa limefanyiwa
maboresho ya hali ya juu.Alisema sanda hizo zimetoka Karachi Pakistan.
Social Plugin