Balozi
wa mtaa wa Mbuyuni uliopo kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga Pius Makonda
amenusurika kufa baada ya kukatwa panga kisogoni na sehemu zingine za mwili
wake na watu wasiojulikana kisha kunyang'anywa mali zake katika Daraja la
Mhumbu lililopo katika barabara itokayo Shinyanga hadi Mwanza.hapa anaonesha sehemu aliyokatwa panga
Balozi
wa mtaa wa Mbuyuniambaye
pia ni Katibu wa Chama cha Wapanda Baiskeli mkoa wa Shinyanga (CHABASHI)
Akizungumza na malunde1.blogspot.com nyumbani kwake
muda mchache baada ya kutoka hospitali ya mkoa wa shinyanga kupatiwa matibabu Balozi
huyo wa mtaa wa Mbuyuni ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Wapanda Baiskeli mkoa
wa Shinyanga (CHABASHI)
alisema tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia leo majira ya saa nne wakati akielekea
nyumbani kwake akitokea mkoani Simiyu kikazi.
Ameongeza kuwa gari alilokuwa anasafiri nalo lilimshusha
njiani,na hakupata tena usafiri ndipo akaanza kutembea kwa miguu na alipofika
eneo la daraja la Mhumbu barabara ya Shinyanga-Mwanza kwenye matuta ya
barabara akavamiwa na vibaka watatu waliokuwa na marungu na mapanga.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Mbuyuni Chifu Abdallah Sube alisema matukio ya watu kukatwa mapanga
yanazidi kuongezeka na imefikia wakati
wananchi wanaogopa kupita kwenye baadhi
ya maeneo kuanzia saa mbili usiku kwa hofu ya kukatwa mapanga.
Alisema hadi
sasa hapo katika daraja la Mhumbu watu
zaidi ya wanne wakiwemo waendesha baiskeli maarufu daladala wamekatwa mapanga na watu wasiojulikana na kuporwa mali
zao hivyo ameliomba jeshi la polisi kushirikiana na wananchi ili kuwabaini
wahalifu.
Kwa upande
wake kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya alisema
jeshi limeanza kufanya msako mkali wa kubaini
waharifu wakiwemo wanaojihusisha na mauaji mkoani shinyanga ambapo jana waliwakamata watu
watatu wakimiliki silaha kinyume cha sheria.
Waliokamatwa ni Musa Mwendo (44) akiwa na
bunduki aina ya shotgun yenye namba 85864 ikiwa na risasi moja,mkazi wa Bugomba
A wilayani Kahama,Andrew Misana (30) Mkazi wa Bugomba B wilayani humo akiwa na
bunduki aina ya gobore ikiwa na risasi zake yaani goroli au malisau 30 pamoja na Melewa
Bugarama(34) mkazi wa Bugamba B,akiwa na magobore mawili na malisau 45.
Social Plugin