Katikati aliyesimama ni
afisa uhamiaji wa mkoa wa Shinyanga Annamaria Yondani ambaye amesema kazi ya
kuwasaka wahamiaji wanaoingia mkoani shinyanga imeshaanza na tayari wamekamata
wahamiaji haramu 18 kati yao 16 wamekamatwa wilayani Kahama na wawili waliochuchumaa wamekamatwa mjini Shinyanga wakiwa ni wahamiaji kutoka nchini KENYA NA RWANDA.
Imedaiwa kuwa wahamiaji hao wengi ni kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Kenya na wengi wao walikuwa wakiishi mikoa ya
Kagera na Kigoma na wanaishi maeneo mbalimbali hapa nchini wakihifadhiwa na jamaa zao.
Social Plugin