Awali mbunge wa jimbo la solwa Mheshimiwa Ahmed Ali Salum akiwasili katika eneo la kikao cha kukabidhi madawati kwa uongozi wa shule ya msingi Bubale iliyopo kata ya Masengwa wilaya ya Shinyanga,alivaa kofia ndiyo mbunge wa solwa akishikana mkono na Mkurugenzi wa wilaya ya shinyanga Mohammed Kiyungi .
Mbunge
wa solwa Ahmed Salum,aliyevaa kofia, hapa mzuka umepanda na akaamua
kuungana na jeshi la sungusungu
kutoa burudani wakati wa kukabidhi madawati 77 ikiwa ni mchango wa jeshi
hilo
kwa kushurikiana na wananzengo wa kijiji hicho cha bubale kilichopo
katika kata
ya masengwa.Lakini mwenye Suti nyeusi ni diwani wa kata hiyo Nicodemus
Luhende akiwa na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya
shinyanga wakitoa wakionesha furaha yao
|
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Eliakim Mathew akizungumza wakati wa kukabidhiwa madawati hayo ambapo alisema shule yake ina wanafunzi 653 na walimu 14 |
Wanafunzi wa shule hiyo wakisoma shairi ambapo walieleza kufurahia kitendo cha wazazi wao kuwapatia madawati |
SAFI SANA NDUGU YANGU ....Mbunge wa solwa na diwani wa masengwa wanakaa katika moja ya madawati yaliyokabidhiwa |
Kushoto ni mwandishi wa radio faraja Geni Elias akichukua mawili matatu katika kikao hicho,kushoto ni mwalimu mkuu wa shule bubale
Wananchi wanafuatilia kinachoendelea |
Social Plugin