ZAIDI YA WATOTO 800 WANAISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI ZAIDI KATIKA KATA YA NDEMBEZI MANISPAA YA SHINYANGA

Afisa maendeleo ya jamii kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga  bi Octavina Kiwone akitoa somo katika semina ya siku moja kwa kamati inayoshughulikia watoto waishio katika mazingira hatarishi zaidi kutoka katika kata hiyo hapo jana katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo,mafunzo mafunzo yalilenga mradi wa TUTUNZANE yakiwa yamefadhiliwa na shirika la Save the Children ambalo afisa maendeleo huyo alisema shirika hilo ni mdau mkubwa sana kuhusu haki za watoto

Afisa mtendaji wa kata ya Ndembezi James Dogani akifuatilia kwa makini somo katika semina hiyo ambapo ilielezwa na afisa maendeleo huyo kwamba kwa mujibu wa zoezi walilofanya la kuhakiki watoto walibaini kuwa zaidi ya watoto 800 wanaishi katika mazingira hatarishi zaidi katika kata hiyo huku kata ya Ndembezi ikiongoza kwa kuwa na watoto waishio katika mazingira hatarishi zaidi kati ya kata 17 zilizopo katika manispaa ya shinyanga
Wajumbe wakisikiliza kilichokuwa kinaendelea katika semina hiyo ilifadhiliwa na shirika la save the children
Somo linaendelea kukolea
hapa wajumbe wakisikiliza vigezo vinavyotumika kuwatambua watoto walioko katika mazingira hatarishi zaidi kwamba ni pamoja na kuangalia hali ya afya ya mtoto,hali ya makazi,hali ya elimu ya mtoto,hali ya lishe ,hali ya ulemavu,hali ya mavazi,hali ya malezi,hali ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya mtoto,ajira na hali ya kisaikolojia kwa mtoto
Hapa washiriki wa semina wanaweka kumbukumbu kuhusu haki za mtoto ambazo ni pamoja na haki ya kuishi,haki ya kuendelezwa,haki ya kulindwa na haki ya kushiriki mfano kupata habari na kutoa maoni
Afisa maendeleo ya jamii kata ya Ndembezi bi Octavina Kiwone akizungumzia kuhusu makundi ya watoto walio katika mazingira hatarishi zaidi kuwa ni pamoja na watoto wenye ulemavu,watoto yatima,watoto walioko katika mikinzano ya kisheria,waishio mitaani,waishio kwenye familia zenye migogoro ya ndoa,waishio katika vituo vya kulelea watoto,wanaofanyishwa biashara ya ngono,wanaopata mimba wakiwa wadogo,wanaoolewa wakiwa na umri mdogo,wanaofanyishwa kazi za hatari,wanaotelekezwa n.k

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post