KIJANA ACHAPWA BAKORA ZA KUTOSHA BAADA YA KUIBA SIMU MSIBANI -NGOKOLO SHINYANGA MJINI

Aliyevaa tisheti nyekundu ni kijana aliyejikuta katika wakati mgumu baada ya kutuhumiwa kuwa ameiba simu 3 usiku wa kuamkia leo katika eneo Bimbo ,Ngokolo mjini Shinyanga.Aliwavizia akinamama wakiwa wamelala jana usiku katika eneo la msiba uliotokea jana katika familia moja eneo hilo. Hapa jamaa anajitetea kuwa hakuiba ila amefananishwa tu.Kulia ni miongoni mwa waliokuwa wanamchapa bakora kijana huyo
Kijana huyo amejulikana kwa jina moja la Fikiri ,ndiyo huyu alituhumiwa kuiba simu,jana usiku amekamatwa mchana huu na kuanza kushushiwa kipigo na wananchi kabla jeshi la polisi  mkoa wa Shinyanga halijafika  kumwokoa muda mchache wakati tukio la kuchapwa bakora likiendelea
Baadhi ya wanachi wakichungulia kilickuwa kinaendelea ndani kwani kijana aliingizwa ndani na kuchapwa bakora

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post