Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla |
Siku chache tu
baada ya hakimu kunusurika kufa baada ya kuchomwa kisu na mlalamikaji katika
kesi moja ya baiskeli mjini Shinyanga,tukio jingine limejitokeza ambapo safari
hii mwalimu wa shule ya msingi Mihama katika kijiji cha Mihama wilayani Kishapu
mkoani Shinyanga ameua mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni jambazi kwa kumchoma mkuki
kifuani baada ya jambazi huyo akiwa na wenzake kuvamia nyumbani kwa mwalimu
huyo.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa saba usiku ambapo mwalimu wa
shule ya msingi Mihama,aliyejulikana kwa jina la Paulo Nahembe(40) akiwa
amelala nyumbani kwake alivamiwa na watu hao wakiwa na marungu,mapanga na
mikuki.
Kamanda huyo ameiambia malunde1.blogspot.com kuwa Mwalimu Paulo Nahembe alianza kupambana na watu hao na kufanikiwa kumchoma mkuki mmoja wao ambaye
hakufahamika jina lake mara moja mwenye umri kati ya miaka 30-35 na akafariki
dunia papo hapo huku wenzake wawili wakifanikiwa
kutoroka na jeshi la polisi mkoani Shinyanga linaendelea kuwatafuta watu hao.
Social Plugin