Semina ya siku 4 kuhusu uandaaji na usambazaji wa habari kupitia njia ya mtandao-ONLINE JOURNALISM yakamilika mjini Kahama
Friday, September 06, 2013
Mchambuzi
wa mfumo wa computer Lukelo Mkami akifundisha namna ya kufungua blog na kutumia
mitandao ya kijamii kwa ajili ya kupashana habari katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na
teknolojia mafunzo ya siku 4 yaliyokamilika jana ALHAMIS mjini Kahama mkoani Shinyanga
Miongoni mwa washiriki wa mafunzo
hayo kushoto ni Suzy Butondo mwandishi wa gazeti la Mwanachi,kulia ni Wezay
Ally kutoka Radio Faraja wakifungua Blog tayari kuanza kuandika habari kwenye
mtandao wa intaneti.
Muda
mchache baada ya mafunzo ya siku nne yaliyoandaliwa na UTPC kukamilika ,hapa ni
ndani ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya
Kahama Benson Mpesya,aliyesimama wa tatu kutoka kushoto ni meneja wa Radio
Kahama Marco Mipawa,mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akimkaribisha mchambuzi
wa mifumo ya kompyuta Lukelo Mkami ili atambulishe rasmi aina mpya ya uandishi
wa habari hapa nchini
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya
wakati wa zoezi la kutambulisha aina hiyo ya uandishi wa habari katika wilaya
hiyo na mkoa wa shinyanga kwa ujumla uliofanywa na mchambuzi wa mifumo ya
kompyuta kutoka muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC Lukelo
Mkami,ambapo mkuu huyo wa wilaya aliwataka waandishi wa habari kuchangamkia
fursa mbalimbali za mafunzo yanayotolewa na muungano wa vilabu vya waandishi wa
habari Tanzanua UTPC hali ambayo
itawasaidia kuongeza ujuzi katika utendaji wa kazi zao na kuongeza kuwa
serikali inatambua sana umuhimu wa waandishi wa habari hapa nchini.
Na
mimi Mkurugenzi wa malunde1.blogspot.com ,Kadama Malunde ,Kushoto nikaamua
kupiga picha na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
,Shija Felician,ambapo aliwataka waandishi wa habari kukubali mabadiliko ya kiteknolojia
Picha
ya pamoja kwa baadhi ya washiriki wa
mafunzo hayo wa pili kutoka kushoto ni mchambuzi wa mfumo wa kompyuta kutoka muungano
wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC Lukelo Mkami,ambaye alikuwa
mkufunzi wa mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uandishi wa habari kwa njia ya mtandao
wa intaneti yaliyodumu kwa siku 4 na kuwakutanisha waandishi 18 kutoka mkoa wa Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin