Idadi ya wanawake wanaoota ndevu mithili ya wanaume inazidi
kuongezeka nchini. Hali hiyo imeshtua pia wataalamu wa afya ambao
wamesema ingawa hakuna takwimu halisi ya wenye tatizo hilo, lakini hali
inatisha.
Uchunguzi uliofanywa kuhusiana na suala hilo umebaini
kuwa hali hiyo inasababishwa na mambo mbalimbali, yakiwemo ya kurithi,
utumiaji mbaya wa vyakula na matumizi holela ya vipodozi.
Daktari Adam Nyalandu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
aliliambia gazeti hili jana kuwa tatizo la wanawake kuota ndevu
linatokana na sababu nyingi ikiwemo matumizi ya vipozi vyenye kemikali
na vyakula vya kusindika.
Alisema matumizi ya vipodozi vya aina tofauti vyenye viambata vya
sumu vimekuwa vikichangia madhara mbalimbali kwa wanawake ikiwemo uotaji
ndevu.
Pia alisema baadhi ya wanawake wamekuwa wakitumia vipodozi vya aina
tofauti ili kutakatisha ngozi zao zionekane kama za wazungu bila kujua
madhara yake. Alisema vipodozi vingi vina viambata vyenye sumu ambayo ni
tishio kiafya.
Dk. Nyalandu alifafanua kuwa baadhi ya vyakula vya kusindika vimekuwa
vikitengenezwa kwa kutumia kemikali nyingi ambazo zinachangia tatizo
hilo kwa wanawake, ambapo madhara yake kwao yameanza kuonekana wazi
wazi.
“Mfano ulikuwa huli nyama za kopo au vyakula vya kusindika ambavyo
kemikali inatumika kuvisindika sasa unakula, vinaweza kusababisha hilo
tatizo hilo kwa kiwango kikubwa,” alisema Dk. Nyalandu.
Alisema ni vema wanawake wakawa makini na vipodozi wanavyotumia kwa
kuchunguza viatamba vya sumu ili kuepuka kuvitumia kwa usalama wa afya
zao. Kwa upande wake, Dk. Abdallah Mandai aliwaonya wanawake na
kuwataka kuachana na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali sanjari na
ulaji wa vyakula vya kizungu.
Alisema wanawake wengi hususan wa mijini wamekuwa wakitumia vipodozi
vyenye kemikali huku wakila vyakula vinavyoandaliwa kisasa zaidi vikiwa
na mafuta mengi au kukaangwa na hivyo kuharibu homoni zao na kusababisha
madhara mbalimbali.
Dk. Mandai alisema matumizi ya vipodozi si tu yana athari ya
kuwafanya wanawake waote ndevu, bali wengi wao wanapopata ujauzito
hujifungua kwa njia ya upasuaji.
“Dawa ya nywele wanayotumia pamoja na vipodozi vyenye kemikali
huchangia kwa kiasi kikubwa kuota ndevu, katika hili la vipodozi tambua
kuwa chochote kinachokuwa juu ya ngozi ya binadamu kina uwezo wa
kusambaa mwilini na kusababisha madhara mbalimbali,” alisema Dk. Mandai.
Akitolea mfano, alisema zamani wanawake wakiwemo wajawazito walikuwa wanakula vyakula vya asili na kwamba walizuiwa hata kula mayai hali iliyokuwa ikiwasaidia wengi wao kujifungua kwa njia ya kawaida.
Akitolea mfano, alisema zamani wanawake wakiwemo wajawazito walikuwa wanakula vyakula vya asili na kwamba walizuiwa hata kula mayai hali iliyokuwa ikiwasaidia wengi wao kujifungua kwa njia ya kawaida.
“Kuna wakati wajawazito 10 wanakuwa wamelazwa hospitali, kati yao
pengine wawili tu ndiyo wanaweza kujifungua kwa njia ya kawaida… wengine
wanafanyiwa upasuaji,” alisema.
Aliongeza kuwa tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi kikubwa iwapo
wanawake watabadilika na kupenda vitu vya asili na kuacha kuiga
utamaduni wa kimagharibi ambao una athari kubwa kwao.
“Ushauri wangu ni kwamba tuache kupeperusha bendera ya umagharibi (kuiga tamaduni za kigeni), tudumishe mila zetu ikiwemo kula vyakula vya asili, matatizo haya yatapungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Dk. Mandai.
“Ushauri wangu ni kwamba tuache kupeperusha bendera ya umagharibi (kuiga tamaduni za kigeni), tudumishe mila zetu ikiwemo kula vyakula vya asili, matatizo haya yatapungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Dk. Mandai.
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia
Simwanza alinukuliwa wakati mmoja akisema mamlaka hiyo imepiga marufuku
vipodozi vyote vyenye viambata sumu, lakini watu wanaendelea kuvitumia.
“Madhara yake ni makubwa, mwanamke mjamzito ni rahisi kuzaa mtoto
taahira, au mimba ikatoka,” alisema huku Daktari wa Magonjwa ya Ngozi wa
Kituo cha Afya Centre, Isaack Maro akisema wanawake wanaotumia vipodozi
vyenye viambata sumu huathirika kwa kiasi kikubwa bila kujijua.
Alisema madini ya zebaki yanayotumika katika vipodozi vingi hayatoki
kwa urahisi mwilini kwani hujazana mwilini kwa muda mrefu na kusababisha
maradhi.
“Watu wanaotumia vipodozi hivyo figo zao huwa zimetoboka kutokana na kuharibiwa na madini hayo,” alisema Dk. Maro.
CHANZO-JAMBOLEO
Social Plugin