ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA KINANA YAANZA KWA KISHINDO SHINYANGA,MAELFU WAJITOKEZA KUMLAKI,CCM YALAMBA WANACHAMA WAPYA ZAIDI YA 500,WAPINZANI NAO WAMO
Wednesday, September 11, 2013
Katikati ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa shinyanga Hamis Mgeja akimkaribisha Katibu mkuu wa CCM taifa Abdulrahman Kinana aliyesimama kulia katika eneo la ofisi ya Kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga muda mchache baada ya kuwasili akitokea mkoani Tabora hapo jana tayari kwa ziara ya siku nne mkoani humo,kuanzia wilayani Kahama,Shinyanga,Kishapu na baadaye Shinyanga manispaa.Kulia ni Katibu wa itikadi,siasa na uenezi CCM taifa Moses Nape Nnauye
Kulia ni Kinana akiwasalimu wananchi wa Kata ya Isaka
Katika viwanja vya CDT mjini Kahama ,kushoto ni Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige akieleza kero za wananchi wa Kahama mbele ya Kinana kuwa ni pamoja na tatizo la umeme ,maji na barabara
Maelfu ya wakazi wa Kahama waliojitokeza kusikiliza Kinana katika viwanja vya CDT mjini Kahama
Siyo kwamba wananchi hawa wako safarini,HAPANA,ni katika eneo la mkutano,wanafanya jitihada za kumuona Katibu mkuu CCM taifa kwani maelfu ya watu walikuwepo eneo hilo la mkutano mjini Kahama
Kinana anapokea wanachama wapya zaidi ya 500 ,wengine ni kutoka vyama vya Upinzani,hapo kashikilia kadi zilizorudishwa na wananchama kutoka CHADEMA NA CUF
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin