Na Valence Robert--.
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la David Aloyce [18] mkazi wa kijiji cha Katolo wilaya ya Geita mkoani Geita amehukumiwa na mahakama ya wilaya ya Geita kutumikia kifungo cha miaka [3] kwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Wakili wa serikali Bi Janne Kisibo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Zabron Kisasi ameiambia mahakama hiyo kuwa tarehe 4/10/2013 David Aloyce akiwa katika kijiji hicho cha katolo kwa nyakati tofauti alijifanya kuwa yeye ni askari polisi na kwamba anaweza kuwapatia ajira watu wa kijiji hicho.
BI Janne alisema kwa kutumia cheo hicho David aliweza kutapeli kiasi cha shilingi laki mbili kwa njia ya m pesa kutoka kwa Sengi Yunvu aliyemtapeli wa laki moja Zakaria Kachila aliyemtapeli kiasi cha shilingi 50,000/ na Leusi Mpayuka aliyetapeliwa shilingi 50,000 akidai kuwapatia ajira kwenye jeshi la polisi na watalipwa mshala mnono.
kutokana na kifungu cha sheria cha [302] cha mwaka 2002 Bi Janne aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa hili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Akijitetea mahakamani hapo mbele ya hakimu Kisasi ,mshtakiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani kuna wazazi na wadogo zake wanamtegemea lakini mahakama ilitupilia mbali ombi lake na kumhukumu miaka [3 ]jela na kila kosa likiwa ni mwaka mmoja mmoja.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin