Na Valence
Robert, Geita
Jeshi la polisi
mkoani Geita limetakiwa kufanya kazi kwa kushirkiana na wananchi ili wananchi
waweze kuwapatia askari taarifa za wahalifu.
kauli hiyo imetolewa leo na naibu kamishina wa
polis Sospeter kondela wakati wa kuzindua bwalo la polisi la mkoa wa Geita katika
makao makuu ya mkoa wa Geita,
Amesema
askari polisi wanatakiwa kushirikiana na wananchi ili kupata taarifa za wahalifu
na sio kuwatisha wananchi.
Aidha
amesema kuna baadhi ya polisi wamekuwa wakiwatishia wananchi na kuwabambikizia
kesi ambapo amesema kama
watabinika watachukuliwa hatua kali.
Pamoja na
mambo mengine amefungua bwalo la polisi
na kutoa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na mgodi wa dhahabu [GGM ] pamoja na wadau mbalimbali kama vile
vitanda vyoo na mahema vyote vikiwa na thamani ya shlinga milioni mia mbili
themanini na sita.
Naye kamanda
wa jeshi la poli mkoa wa Geita Leonard Paulo aliwashukuru wadau pamoja na mgodi
huo [GGM] kwa msaada walioutoa na kwamba wananchi wa mkoa wa Geita kwa
kuendelea kutoa ushirikiano na mzuri na
kuwafichua askari wanaowasunbua.
Kwa upande
wake mkurugenzi wa mgodi wa [GGM] Bw Michael Van alisema wameamua kutoa misaada
hiyo kwasababu ya ushirikiano uliopo kati ya polisi na mgodi na kuahidi kuendelea
kulisaidia jeshi hilo
na wasisite kuomba msaada pale wanapohitaji,
Social Plugin