Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla |
Kijana mmoja aitwaye Juma Masasila 25-30 ameuawa kwa kushambuliwa
na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa mawe baada ya
kuvamia nyumba ya mkazi mmoja katika kijiji cha Lunguya tarafa ya Msalala wilaya
ya Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
ACP Evarist Mangalla kwa vyombo vya habari tukio hilo limetokea tarehe 13
Octoba mwaka huu majira ya saa tano na nusu usiku ambapo Juma Masasila
aliuawa kwa kushambuliwa na wananchi kwa kumpiga mawe na fimbo sehemu mbalimbali
za mwili wake na kusababisha kifo chake papo hapo.
Chanzo cha mauaji hayo kuwa ni kitendo cha marehemu kuvamia
nyumbani kwa bwana Amos Makoye kwa nia ya kumkata panga ndipo mkazi huyo
alipopiga kelele kuomba msaada hali iliyosababisha wananchi kufika eneo
la tukio na kuanza kumshambulia marehemu.
Kamanda Mangalla amesema katika eneo la tukio kuliokotwa panga moja na
kisu vitu ambavyo vinasadikiwa kuwa ni silaha alizokuja nazo marehemu kwa ajili
ya kumcharanga bwana Amos Makoye na kuongeza kuwa hakuna mtu aliyekamatwa
kuhusika na tukio.
Social Plugin