KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA

Aliyesimama ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC),bwana Shija Felician akizungumza leo wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo ambao umefanyika katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alikemea vikali tabia ya baadhi ya wanachama wake kukiuka maadili ya kazi ambapo baadhi yao wanatumia lugha chafu na kuendekeza pesa badala ya kazi na kusababisha kero katika jamii

Mkutano unaendelea
Mweka hazina  wa SPC bi Stella Ibengwe akisoma taarifa kuhusu mapato na matumizi ya klabu hiyo kwa mwaka 2013
Picha ya pamoja ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambapo sasa wamefikia 32 baada ya
mkutano huo mkuu wa mwaka kumepokea majina ya wanachama wapya 9 walioomba uanachama ambao tayari kikao cha kamati tendaji kilikuwa kimewapitisha nao  ni Bi Lucy Masalu,Paulo Kayanda,Happiness Kihampa,Herieth Katikiro,Neema Mghen,Shangwe Than,Geni Elius na Michael Maduhu na bwana Kadama Malunde ambaye ndiyo mkurugenzi wa blog hii ya malunde1.blogspot.com.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post