Mwanamke aliyejulikana kwa jina laVeronica Stephano (25)
mkazi wa kijiji cha Idukilo kata ya Mwadui wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
ameuawa kunyongwa na mme wake aitwaye Salawa Nhela(35) na baada ya kumuua mke wake naye akajinyonga.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Shinyanga Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea leo majira
ya saa moja asubuhi ambapo mwanamke huyo amekutwa amefariki dunia kitandani baada ya kunyongwa na mume wake na
baada ya mwanamme huyo kufanya tukio hilo naye aliamua kujinyonga kwa
kutumia kamba ya katani juu ya dali ndani ya chumba chao.
Amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni
wivu wa mapenzi kufuatia mwanamme kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wanaume wengine na kuongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Social Plugin