kijana
mwingine ameuawa kwa kupigwa mawe na kisha mwili wake kuchomwa moto na wananchi
baada ya kutuhumiwa kuiba kuku wanne katika kijiji cha Mawimilu kata ya
Mwakitolyo tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla tukio hilo limetokea Octoba 17
mwaka huu jioni ambapo kijana
asiyefahamika jina wala makazi yake mwenye umri wa miaka kati ya 25-30
aliuawa kwa kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mawe na fimbo kisha mwili wake kuchomwa
moto baada ya marehemu kutuhumiwa kuiba kuku wanne ingawa hata hivyo wamiliki wake
hawajafahamika.
Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya kijana mwingine wilayani Kahama kuuawa na wananchi baada ya kuvamia nyumba ya mtu akiwa na panga na kisu.
Social Plugin