Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla |
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawatafuta watu
waliohusika na mauaji ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Misoji Kasubi
(50) mkazi wa kijiji cha Manhigana kata ya Solwa tarafa ya Nindo, wilaya ya Shinyanga vijijini ambaye ameuawa kikatili kwa kukatwa panga kichwani,mdomoni na bega la kushoto wakati
akitoka kujisaidia nje ya nyumba yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist
Mangalla amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa saba na nusu usiku na
mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana na uchunguzi kuhusu tukio
hilo unaendelea.
Social Plugin