Kikongwe mmoja aliyejulikana kwa jina la Kabula Nkanda (55) mkazi wa kijiji cha Mwadui -Luhumbo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ameuawa kikatili baada ya kucharangwa mapanga na watu wasiojulikana muda mchache tu baada ya kutoka harusini.
Tukio hilo limetokea jana Oktoba 28,majira ya saa mbili usiku katika kitongoji cha Luhumbo C katika kijiji hicho cha Mwadui –Luhumbo kata ya Mwadui-Luhumbo na kuongeza kuwa mwanamke huyo alivamiwa na watu wasiojulikana na kumcharanga mapanga sehemu za kichwani,mkono wa kushoto na sehemu ya titi lake la kulia na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kaimu afisa mtendaji wa kata ya Mwadui-Luhumbo bwanaWillium Masali amesema chanzo cha mauaji hayo huenda kinatokana na imani za kishirikina kutokana na kwamba marehemu alikuwa anatuhumiwa kumuua kishirikina mke wa mkazi mmoja wilayani humo aitwaye Jilungu Bulugu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa atatoa baadaye taarifa kamili kuhusu tukio hilo
Social Plugin