NB haya ni makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga |
Na Valence Robert,Geita
Siku chache tu baada ya
mtoto kudaiwa kufufuka hofu imezidi
kutanda miongoni mwa wakazi wa mkoa wa Geita,ambapo mtu mwingine anayedaiwa kufariki dunia zaidi
ya mwaka mmoja uliopita kuonekana akiwa hai huko katika kijiji cha Rumasa kata
ya Buseresere wilaya ya Chato mkoani Geita.
Mtu huyo anayefahamika kwa jina la Mgonda Thomas (22) ambaye
anasemekena kuwa alifariki dunia Mei 28,mwaka jana,ameonakana akiwa hai juzi
majira ya saa 9 alasiri wakati akitembea barabarani jirani na nyumbani kwao.
Imeelezwa kuwa majirani
walipomuona walimtambua kwa sura mtu huyo
na baadaye waliamua kutoa taarifa
kwa ndugu zake wakiwemo wazazi wake ambao ni Thomas Msalaba (60) na Martha
Kitobelo ambapo walipomuona nao walimtambua kwa sura na alama ya kovu la mkono
wa kushoto lilitokana na kuungua kwa moto wakati wa uhai wake.
Kufuatia tukio hilo la
kushangaza ndugu zake walimchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji Juma
Tabiho umbali wa kilomita moja kutoka nyumbani kwao kutokana na kulihusisha
tukio hilo na imani za kishirikina.
Hata hivyo jeshi la
polisi wilayani Chato likiongozwa mkuu wake wa wilayani humo, Leonard Nyaoga
lililazimika kufanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi waliotaka kufukua kaburi
kujua kilichomo ambapo baadaye askari walimchukua na kumpeleka kituoni kwa
maojiano zaidi.
Tukio hilo limetokea
ikiwa ni wiki mbili baada ya mtoto Shaaban Maulidi(16)aliyefariki dunia mwaka
2011 kuonekana akiwa hai septemba 28,mwaka huu katika Mtaa wa 14 Kambarage mjini
Geita.
Social Plugin