Katibu mkuu wa kanisa la AICT dayosisi ya Shinyanga mchungaji Yakobo Mapambano akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana jioni |
Hatimaye uongozi wa kanisa la AICT dayosisi ya Shinyanga limetangaza jumla ya fedha zilizopatikana katika harambee iliyoendeshwa na mbunge wa jimbo la Sengerema William Ngeleja kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari Bishop Nkola inayomilikiwa na kanisa hilo.
Katibu mkuu wa kanisa la AICT dayosisi ya Shinyanga mchungaji Yakobo Mapambano amewaambia waandishi wa habari kuwa lengo lilikuwa ni kupata milioni 350, na jumla ya pesa katika changizo zilizopatikana mpaka sasa ni shilingi milioni 263,laki 2,elfu 4 na mia tisa
Katika harambee hiyo kanisa lilipokea michango kutoka kwa Prince Mobutu(mtoto wa rais wa zamani wa Zaire Mobutu Seseseko),askofu mkuu wa AICT nchini Kenya Silas Yego,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nasoro Rufunga,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi,mwenyekiti wa CCM mkoa wa shinyanga Hamis Mgeja,mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele,mbunge wa viti maalum Rachel Mashishanga na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Social Plugin