Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAKAMANDA WA SUNGUSUNGU WAFUNGUKA,WASEMA NDALA INAONGOZA KWA UHALIFU,IKIFUATIWA NA NDEMBEZI NA NGOKOLO KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA

Kamanda mkuu wa sungusungu tawi la Tambukaleli katika manispaa ya Shinyanga bwana John Tulla akizungumza JANA wakati wawa kikao cha jeshi la jadi (sungusungu) kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga ambayo inachukua nafasi ya pili kwa uhalifu kama vile wizi wa baiskeli,ng’ombe,kuku na vitu mbalimbali katika manispaa hiyo huku kata ya Ndala ikiongoza na Kata ya Ngokolo ikichukua nafasi ya tatu kwa uhalifu

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbuyuni bwana Chifu Abdallaha Sube akizungumza wakati wa kikao hicho cha makamanda wa sungusungu ambapo alisema kuna baadhi ya askari polisi sio waaminifu kwamba wanashirikiana na wahalifu kwani baadhi yao wamekuwa wakishuhudia uhalifu ukifanyika bila kuchukua hatua hivyo kusababisha uhalifu kuendelea kushamiri katika jamii

wajumbe wa kikao wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

kikao kinaendelea

Mkaguzi msaidizi wa polisi,polisi tarafa,tarafa ya Shinyanga Mjini Deodatus Rutta ambapo alisema kuongezeka kwa uhalifu katika jamii kunatokana na wanajamii kuwa na uoga wa kuwafichua wahalifu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com