INASIKITISHA !!! KIJANA AFARIKI DUNIA JUU YA MTI SHINYANGA
Monday, October 14, 2013
Mwili wa marehemu George Kwilasa Maswizilo (33)ukiwa juu ya mti unaouona hapo katikati.Ni vigumu kuuona vizuri kwani nguo alizokuwa amevaa zinafanana na mti .Kijana huyo amefariki
dunia papo hapo jana saa mbili asubuhi juu ya mti wakati akikata moja ya tawi la mti huo katika eneo la mtaa wa Mabambasi kata
ya Ndembezi Mjini shinyang.Unaowaona hapo ni baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo la aina yake
ambapo marehemu baada ya kukata mti huo
ulimwamgukia na kumbana tumboni hali iliyosababisha apoteze maisha yake papo
hapo huku akiwa juu ya mti
Mwili wa marehemu ukiwa juu ya mti umebanwa na moja ya tawi la mti aliokuwa anaukata,alikuwa amepewa ujira wa kukata mti huo ikiwa ni ajira inayomwingizia kipato kila siku.Kufuatia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa huyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Ndembezi bwana David Nkulila kwa kushirikiana na wananzengo wa mtaa huyo walifanya mchango kwa ajili ya gharama za mazishi ya marehemu japokuwa sio mkazi wa mtaa huo(marehemu ni mkazi wa Kitangiri mjini Shinyanga na kazi yake hapo mjini ni kukata miti) na bahati mbaya amepoteza maisha akiwa kazini nje ya eneo alikokuwa anaishi.Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin