Na Valence Robert, Geita.
Zaidi ya mawakala
1200 wa Vodacom m-pesa kutoka mkoa
wa Geita wamepewa mafunzo kuhusu jinsi
ya kuwahudumia wateja wao pamoja na mbinu za kuepukana na matapeli waliotapaa katika mkoa mzima wa Geita wanaojitambulisha
kuwa wao ni wafanyakazi kutoka kampuni ya Vodacom.
Akizungumza katika semina
hiyo ya siku moja iliyofanyika jana
katika ukumbi wa Bwalo la polisi mkoa wa Geita mwezeshaji wa mafunzo hayo bwana
Biseco kutoka makao makuu ya kampuni ya Vodacom
jijini Dar es salaam amesema lengo kubwa la mafunzo hayo ni kuwafundisha mawakala hao kuhusu namna
ya kuhudumia wateja na kuepukana na matapeli
wanaojitokeza.
Bwana Biseco amesema kuna matapeli wanaotapeli watu kwa kutumia
jina la mpesa huku wakijitambulisha kuwa
wao ni wafanyakazi wa kampuni ya vodacom
wakati sio kweli na hivyo kuwatapeli mawakala hao.
Amewataka mawakala kuacha kununua laini za [ TILL] mitaani na kwa
wale mawakala wanaouza [TILL] wakibainika watapelekwa mahakamani kujibu mashitaka yatakayowakabili.
Naye meneja masoko
mkoa wa Geita Julius Peter amewataka mawakala na wateja wote wa mkoa Geita kuwa
makini wanapopewa huduma na kutoa huduma kwani matapeli wamekuwa wengi sana
katika mkoa mzima wa Geita na wawaepuke matapeli hao.
Kwa upande wao mawakala
kutoka wilaya tano za mkoa mzima wa Geita ambazo. ni Geita, Chato, Mbogwe, Bukombe
na Nyagware wameshukuru sana kampuni ya Vodacom kwa kutoa mafunzo hayo na kuahidi kutoa huduma kwa uangalifu na
umakini zaidi ikiwa ni pamoja na
kuepukana na matapeli waliotapakaa mkoa mzima wa Geita kwa kujiita
watumishi wa vodacom m –pesa.
Social Plugin